Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, amewaagiza Polisi Mkoani humo kuyaondoa mabango yote ya waganga wa jadi yaliyobandikwa mitaani yakiwemo yanayoeleza kuhusu kuongeza nguvu za kiume kwa madai kuwa yanawaingiza Wananchi kwenye majaribu ya kishirikina.

RC Chalamila amesema baada ya kuyaondoa mabango hayo, uanze mchakato wa kuwakamata waganga wa jadi wote wanaokiuka taratibu za Nchi na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola.

Mchungaji amuua mkewe wakati wa ibada, naye ajichinja

“Vijana wetu wameingia kwenye mitego ya ajabu, wanafikiri nguvu za kiume zinapatikana kwa Waganga mwisho wa siku wanaharibu miili yao na wanaingia kwenye ushirikina ambao hauna maana”

Hivi karibuni, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alitangaza kuanza kuhakiki madhehebu yote ya dini na kuliagiza jeshi la polisi kuwasaka na kuwabaini waganga wote wa kienyeji na kuwakamata wanaoenda kinyume na utaratibu baada ya kuibuka mama anayedhaniwa kuwa ni mchawi kuiba watoto wawili wa familia moja.

Baba kizimbani kwa kukeketa watoto wake
Video: Sinema wizi vifaa Nida, Mbunge CCM adaiwa kuibiwa mil.440

Comments

comments