Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla amewaelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam kuja na mpango mkakati wa kuendeleza soko la Machinga Complex ili Soko hilo liwe kimbilio kwa wamachinga na wateja.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo alipotembelea Soko hilo na kusikiliza kero za wafanyabiashara sokoni hapo, ambao wamemueleza sababu zinazopelekea wafanyabiashara kulikimbia Soko hilo na kwenda mitaani.

Miongoni mwa Kero zilizotolewa na Wafanyabiashara hao ni mazingira mabovu ya kufanya biashara, Utaratibu mbovu wa kupata vizimba, kodi kubwa, Sheria kandamizi, ushirikiano mbovu wa viongozi, umeme, maji, vyoo, maji taka, miundombinu isiyo rafiki na utaratibu wa kulipa kodi ya mwezi badala ya ushuru wa siku.

Kutokana na malalamiko hayo, RC Makalla amewaelekeza Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Jiji kuhitisha vikao vya mara kwa mara na Wafanyabiashara hao na kupeana mrejesho wa utatuzi wa kero zao ili mwisho wa siku biashara zifanyike na serikali ipate mapato.

Aidha, ameelekeza Viongozi wa soko hilo kuachana na tabia ya kufungia biashara za wapangaji wanaoshindwa kulipa kodi na badala yake wakae mezani kuangalia namna Bora.

Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza Halmashauri ya Jiji kufuatilia fedha za NSSF zilizotolewa kama mkopo wa Ujenzi wa jengo hilo lili kujua Kama mkopo umemalizika au bado deni lipo.

DPP awaachia huru watuhumiwa 14
Kumbilamoto: Serikali imefikia muafaka kutatua changamoto hii