Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amezitaka Halmashauri za Mkoa huo kuhakikisha zinafanya shughuli kwa weledi ili kuepuka kashfa za hati chafu au hati za mashaka kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG).

RC Makalla amesema hayo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani Ilala kilichoketi leo Juni 16, 2021 kupitia ripoti ya CAG ambapo amesema ni vyema Halmashauri hizo zikawapatia ushirikiano wa kutosha wakaguzi kwa kuonyesha vielelezo vinavyohitajika.

Aidha RC Makalla ameipongeza Manispaa ya Jiji la Ilala, kwa kupata hati safi kwa miaka mitano mfululizo na kuitaka ifanyie kazi maelekezo na maagizo yaliyotolewa na CAG na Kamati ya Kudumu ya Bunge huku akiwataka kuwatumia vizuri wakaguzi wa ndani.

Pamoja na hayo, RC Makalla amewataka Madiwani kusimamia kikamilifu miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha miradi inaendana na thamani ya pesa.

Hata hivyo RC Makalla ametaka watumishi wote waliosababisha dosari wawajibishwe kwa mujibu wa sheria pasipo uonevu.

Hakuna Hijja mwaka huu
Mahakama yamuachia huru Seth wa ESCROW