Real Madrid na VFL Wolfsburg zimekua timu za kwanza kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu wa 2015-16.

Real Madrid wakicheza katika dimba lao la Santiago Bernabeu mjini Madrid nchini Hispania, waliibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya As Roma, ambayo yalikwamishwa wavuni na Cristiano Ronaldo aliyefunga bao lake la 40 kwa msimu huu, na bao la pili likifungwa na James Rodriguez.

Substitute Lucas Vazquez attempted a series of stepovers before delivering for Cristiano Ronaldo to finish with ease against the Italians

James Rodriguez smashed straight through the legs of Roma goalkeeper Wojciech Szczesny to double the home side's lead on the night

Madrid wanasonga mbele wakiwa wamepata ushindi wa jumla wa mabao manne kwa sifuri, baada ya kujiweka vyema katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa mjini Roma nchini Italia majuma mawili yaliyopita kwa kuibuka kidedea kwa ushindi wa mbili, sifuri.

Kwa upande wa wawakilishi wa Ujerumani VFL Wolfsburg, wamesonga mbele kwa kuwachapa KAA Gent bao moja kwa sifuri, lililofungwa na mshambuliaji Andre Schurrle.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza VFL Wolfsburg walishinda kwa mabao matatu kwa mawili.

Hii leo michuano hiyo iliyo kwenye hatua ya 16 bora, itaendelea tena kwa michezo miwili kuchezwa, ambapo Zenit St. Petersburg watakua nyumbani kwao nchini Urusi wakiwakabili Benfica kutoka nchini Ureno.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza Benfica wakiwa nyumbani nchini Ureno waliibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri.

Mchezo mwingine wa hii leo utakua kati ya mabingwa wa soka wa nchini England, Chelsea ambao watawakaribisha Paris Saint Germain kutoka Ufaransa kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza ambao ulifanyika nchini Ufaransa, Paris Saint Germain walifanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao mawili kwa moja.

Eva Carneiro Aendeleza Vita Na Jose Mourinho
Maalim Seif atoa ya moyoni baada ya kutoka Hospitali