Hatimae uongozi wa klabu ya Sunderland, umekamilisha mpango wakumpata mrithi wa Dick Advocaat aliyetangaza kuondoka klabuni haopo mwishoni mwa juma lililopita.

Sunderland, wamemtangaza aliyekua meneja wa klabu za Bolton Wanderers, Newcastle Utd pamoja na West Ham Utd, Sam Allardyce.

Allardyce, anakwenda Stadium of Lights baada ya kukubali kusaini mkataba wa miaka miwili, huku akitarajiwa kufanya mapinduzi ya kisoka kwenye kikosi cha klabu hiyo ambacho kilianza vibaya msimu huu.

Allardyce, mwenye umri wa miaka 60, amepewa ajira ya kukiongoza kikosi cha Sunderland kutokana na ufanisi wake kuonekana unafaa na kuwazidi mameneja wengine, ambao walikua wakipigiwa upatu wa kuchukua mahala palipoachwa wazi na Advocaat ambaye alioneka kushindwa kufikia lengo.

Baada ya kuthibitishwa kuwa meneja wa klabu ya Sunderland, meneja huyo kutoka nchini England alizungumza kwenye kituo cha televisheni cha klabu hiyo, na kuelezea furaha yake ya kurejea katika tasnia ya ufundishaji soka, huku akionyesha kuwa na uchu wa kuleta changamoto mpya ya ushindani.

Amesema, anatambua wajibu ulio mbele yake, na bila ajizi atajitahidi kadri awezavyo ili kufanikisha malengo yanayokusudiwa  na viongozi wa Sunderland ambao walionyesha kuchoshwa na hali mbaya iliyokua inawanyemelea.

Hata hivyo histoaria inaonyesha, Allardyce aliwahi kupita Sunderland kama mchezaji kati ya mwaka 1980-81 na baada ya hapo alijiunga na mahasimu wa The Black Cats, Newcastle Utd.

Mtihani wa kwanza kwa Sam Allardyce, utakua mwishoni mwa juma hili ambapo kikosi cha Sunderland kitasafiri kwenda The Hawthorns  kuwakabili wenyeji wao West Bromwich Albion.

Samatta kuwania Tuzo Ya Afrika
Unashindwa Kuweka Akiba Ya Kipato Chako Kidogo? Tumia Njia Hizi