Serikali imemjibu kwa vitendo Mbunge wa Mbulu Vijijini, Fratei Massay ambaye alilazimika kuruka sarakasi Bungeni, ili kufikisha ujumbe wake wa kujengewa barabara, kwa kuanza ujenzi huo kwa kiwango cha lami.

Mei 23, 2022 katika vikao vya Bunge, akichangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Massay aliruka sarakasi kushinikiza kujengwa kwa barabara inayopita jimboni kwake ikitokea Karatu – Mbulu – Singida.

Mbunge wa Mbulu Vijijini, Fratei Massay.

Barabara hiyo, imetengewa kiasi cha Shilingi 37 Bilioni kwa ajili ya ujenzi wa kilomita 25 ambazo zinahusisha kipande kinachotoka Hydom hadi Laban huku mbunge huyo akiitaka Serikali kumpelekea fedha Mkandarasi ili aongeze kasi ya ujenzi.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi – CCM, Daniel Chongolo ameiagiza Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuongeza urefu wa barabara hiyo kutoka kilomita 25 hadi 50 na ihakikishe mkandarasi analipwa fedha za ujenzi.

Nabi ataja mbinu za kuizabua AS Real Bamako
Sakata la Fei Toto, Ally Kamwe apiga kwenye mshono