Tanzania imefuzu kwa mara ya kwanza kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana U-17 zitakazofanyika Gabon mwaka huu.
Serengeti Boys imefuzu baada ya kushinda rufaa yake dhidi ya Congo iliyo mchezesha mchezaji aliyezidi umri.
Tanzania itaingia Kundi B ikichukua nafasi ya Congo kundi hilo lina timu za Niger, mabingwa watetezi Mali na Angola.
Timu nne zinazofanikiwa kuingia katika nusu fainali zitafuzu moja kwa moja  Kombe la Dunia la Fifa U17 litalofanyika India baadaye mwaka huu.
Waziri wa Michezo, Nape Nnauye ametoa pongezi kwa kuandika kwenye akaunti yake ya twiter kuipongeza Serengeti Boys kwa kufikia hatua hiyo.
“Mungu Mkubwa! Tumefuzu kwenye fainali za Afrika chini ya umri wa miaka 17. Nia, uwezo na sababu za kuchukua kombe hili tunazo. Hongera TZ” amesema Nape

Video: Siri gomvi la DPP, AG hadharani, Makonda ataja vinara
Dkt. Shein asimamia kauli yake kwa watumishi wa umma