Timu ya Mpira wa Miguu ya vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imefanya kambi yake kwa mafanikio huko jijini Victoria kwenye Kisiwa cha Mahe, nchini Shelisheli baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya dhidi ya Northern Dynamo.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Taifa wa Shelisheli, bao pekee la Serengeti Boys lilifungwa na Muhsin Makame katika dakika 75 ya mchezo huo uliokuwa na ushindani mkali katika vipindi vyote viwili kutokana na kushambuliaana mara kwa mara.

Serengeti Boys ambayo ilikuwa na kikosi cha nyota 21 na viongozi watano, wamemaliza kambi ya huko Shelisheli na hivyo inaondoka jioni ya leo Septemba 13, 2016 saa 11:00 jioni na ikitarajiwa kuingia nchini usiku wa saa 7:45 Septemba 14, 2016 ambako itakuwa kambini hadi siku ya mchezo Jumapili Septemba 18, mwaka huu.

Mchezo huo wa kuwania kucheza fainali za kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17. Fainali hizo zitafanyika jijini Antananarivo, Madagascar hapo Aprili, 2017.

Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Nyundo  Shime maarufu kwa jina la Mchawi Mweusi, amesema: “Sitaki kuwa na maneno mengi. Nataka Watanzania waje kuona wenyewe. Maana maneno maneno yakizidi inakuwa kama kero. Nataka kujenga utamaduni wa Watanzania kuja wenyewe uwanjani kuona timu yao.”

Katika hatua nyingine, wapinzani wa Serengeti Boys wanatarajiwa kutua Alhamisi wakiwa na kikosi cha watu 40 na kati ya hao ni 22 ni wachezaji. Miongoni kwa kundi hilo pia kuna wanahabari wanne.

Katika orodha ilitumwa TFF, wachezaji wa timu hiyo ni pamoja na Mathieu Lee Valtair, Balou Prince Joel, Bopoumela Chardon, Kiba Konde Ridrique, Kibasila Christ Benilde, Langa Lessen Bercy, Makouana Beni, Mantouari Juste Aldo, Mata Thomas, Mbemba Patchely Rael, Mbenza Kamboleke, Mboungou Prestige, Mebeza Egouep Craiche, Mouandza Mapata, Moungala Ikounga, Mountou Edouard, Ngakosso oko Alves, Ngaloukossi Jossy Ronel, Nguienda Mouanga Bernice, Nguimbi Exau, Ntoto Gedeon, Oboua Danish na Otang Jeordon.

Viongozi wa timu hiyo wamo Ntoto Lacombe ambaye ndiye Mkuu wa Msafara, Goma Ambroise Stephane ambaye ni Mratibu wa msafara, Ngami Gobard – Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Congo – Brazzavile.

Wengine ni maofisa mbalimbali Otende Charles, Moussavou Merrile, Badji Mombo, Berrettini Paulo, Ekariki Basile, Cesana Eraldo, Bakoua Loufouma Narcisse, Okandze Elenga Jean Pierre, Lounou Joste Feller, Mabila Kengue Francois, Loemba Jean Rufin, Mendome Ndoum, Batangounna Ntari na Mbemba Gervais.

Kilimanjaro Queens Yatangulia Nusu Fainali
Video: TFF yatoa ufafanuzi kuhusu ratiba VPL, yamaliza msuguano na Azam FC