Kufuatia sintofahamu ya nyongeza ya mishahara iliyoridhiwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Mei 14, 2022, Serikali imewataka Wafanyakazi kuwa watulivu na kuahidi kutoa ufafanuzi kuhusu nyongeza hiyo.

Kwa mujibu wa ya Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa aliyoitoa kupitia ukurasa wa Twitter Julai 22, 2022 imesema Wafanyakazi wanatakiwa kutulia kwakua itatolea ufafanuzi wa nyongeza ya mishahara iliyotokea katika mishahara ya Julai, 2022.

“Ndugu wafanyakazi naomba tutulie, Serikali itatoa ufafanuzi kuhusu nyongeza ya mishahara iliyotokea katika mishahara ya mwezi Julai, 2022,” amesema sehemu ya taarifa ya msemaji wa Serikali Gerson Msigwa.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa.

Rais, Samia aliridhia mapendekezo ya kuongeza mishahara ikiwemo kima cha chini kwa watumishi wa umma kwa asilimia 23.3, ambayo ingeanza kufanya kazi katika mshahara wa mwezi Julai.

Mapendekezo hayo, yalikuwa ni mwendelezo wa kikao cha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alichokifanya jijini Dodoma na kupokea taarifa kutoka kwa wataalamu kuhusu ongezeko la mishahara.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus ilisema Serikali imepanga kutumia Sh9.7 trilioni katika mwaka wa fedha 2022/23 kwa ajili ya kugharamia malipo ya mishara ya watumishi wa taasisi na wakala za Serikali, Serikali za Mitaa na Serikali Kuu.

Tweet ya Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa.

IGAD yaonya ujio wa baa la njaa Africa
Shehena nafaka za Ukraine 'ruksa' kupita Bahari nyeusi