Waziri ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima amewaagiza Viongozi na Watendaji wa ngazi zote kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kuhakikisha kuwa wananchi wanaelimishwa kwenda kupata chanjo ili kujikinga dhidi ya UVIKO-19.

Ameyasema hayo leo Novemba 23, 2021 baada ya serikali kupitia wizara hiyo kupokea Dozi 499,590 za Pfizer ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wa Serikali wa kuwakinga Wananchi dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19.

Hafla fupi ya mapokezi imeongozwa na Waziri wa Afya Dkt. Gwajima katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam  na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Serikali, Ubalozi na Taasisi zisizo Zakiserikali.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt.  Gwajima amesema, Serikali kupitia Wizara ya Afya imelenga kuwakinga jumla ya Watanzania 249,795 kutokana na kupokea Chanjo dozi 499,590 za Pfizer zilizoingia kutoka Marekani kupitia mpango wa COVAX Facility.

“Leo Novemba 23, 2021 tumepokea dose 499,590 za Pfizer ambazo zitakinga watanzania 249,795 (dose mbili).” Amesema Dkt. Gwajima.

“Chanjo hizi kama zilivyokuwa za Janssen na Sinopharm zimethibitishwa na WHO kuwa ni bora na salama, huku akisisitiza  Wizara ya Afya itafanya wajibu wake wa kujiridhisha na uhakiki wa ubora wa Chanjo hii kwa kupitia wataalamu wa ndani na Mamlaka husika kabla ya kuanza kutolewa kwa Watanzania,” Amesema Waziri Gwajima

Hadi kufika kufikia tarehe 19.11.2021, takwimu zinaonesha kuwa jumla ya wananchi ,359,624 tayari wamepata chanjo ya kuwakinga dhidi ya UVIKO-19.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa huduma  za Afya na Ustawi wa Jamii na Lishe OR TAMISEMI Dkt. Paul Chawote amewashukuru Wadau kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha afya ya wananchi, huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao katika kuketa Maendeleo hususan katika sekta ya afya.

Rais Samia aja na suluhu ajali za barabarani
Mosimane amkingia kifua Luis Miquissone