Serikali ya Ethiopia, imethibitisha kushiriki mazungumzo ya amani ya wiki ijayo, yatakayoongozwa na Umoja wa Afrika AU, kujaribu kutatua vita vilivyodumu kwa takriban miaka miwili huko Tigray.

Wito wa kimataifa, wa kusitishwa kwa vita kaskazini mwa Ethiopia umezidi kuongezeka tangu juhudi za Umoja wa Afrika ziliposhindwa mapema mwezi huu kuzikutanisha pande zinazozozana kwenye meza ya mazungumzo.

Kundi la wapiganaji huko Tigray. Picha: gq-magazine.co.uk

aIDHA, chama cha ukombozi wa watu wa Tigray TPLF, kimedokeza kuwa kiko tayari kushiriki mazungumzo hayo yanayosimamiwa na Umoja wa Afrika, huku Umoja wa Mataifa UN ukionya uwepo wa hali mbaya eneo hilo la Tigray.

Mapema wiki hii, Serikali kuu ilitangaza kutekwa kwa miji mitatu katika jimbo la Tigray ambako wanajeshi wa taifa hilo na washirika wake kutoka taifa jirani la Eritrea wamekuwa wakiendesha oparesheni dhidi ya waasi wa TPLF.

Augustine Okrah aitaka Game ya Young Africans
Tshabalala: Wao wenyewe watashangaa