Sheria ya usalama barabarani ya mwaka 2014 inatarajiwa kuwa mwarubaini wa kuwatoa barabarani madereva wanaovunja Sheria hiyo.

Sheria hiyo imehalalisha kuanza kutumika kwa mfumo wa kielekroniki kutunza kumbukumbu ya makosa ya dereva kwa kutumia kadi maalum ya dereva husika. Pia, imeanzisha utaratibu unaomuwezesha dereva kulipa faini kwa njia ya kielekroniki bila kumpa askari fedha.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na kampuni Ya Matrix iliyopewa kazi ya kuratibu mfumo huo, dereva atalipa fedha kupitia huduma za  Simu pesa au kuchanja kadi yake ya benki kwenye mashine maalum ya malipo.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, taarifa za makosa ya dereva zilizohifadhiwa kwa njia ya kielekroniki zitapewa ‘points’, na itakapofika kiwango fulani cha point zilizozidi ukomo, leseni ya dereva husika itasitishwa ‘automatically’.

 

Magufuli awatoa sakafuni wagonjwa 300 Muhimbili
Zitto Kabwe Atoa 'Maksi' zake kwa Magufuli