Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu amewataka madiwani wa jimbo hilo waliochaguliwa kwa tiketi ya Chadema kuhakikisha wanafanya kazi kubwa kushindana na kazi ya rais John Magufuli.

Sugu alitoa kauli hiyo hivi karibuni katika kikao cha kumchagua diwani atakayewania nafasi ya Umeya kwa tiketi ya chama hicho.

Aliwataka madiwani hao kuchapa kazi na kuwafanya wananchi kujivunia kasi ya maendeleo inayoletwa na Mbunge na Meya wa jiji hilo ili wasitamani jimbo hilo lingeongozwa na wapinzani wao wa CCM.

“Hata CCM wenyewe wamebadilika, Magufuli anakwenda jalamba. Hakutakuwa na vitu kama ambavyo mnaviwaza, tunaenda kufanya kazi za wananchi ili wananchi wasitamani kwamba afadhali na hapa pangekuwa CCM. Waseme hata kama Magufuli anaenda spidi na sisi Mbeya yetu Meya na Mbunge wanakwenda spidi.”

FIFA Yaendelea Kutikiswa Na Jeshi La Polisi Uswiz
Baadhi ya Watumishi Wa TRA Wakutwa Na Mamilioni Nyumbani Kwao