Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph ‘Sugu’ Mbilinyi, ameingia katika hatari ya kushushiwa adhabu kali baada ya kudaiwa kuwatusi wabunge wa CCM kwa kuonesha alama ya vidole.

Sugu alidaiwa kuonesha kidole cha kati kinachotafsiriwa kuwa tusi wakati Wabunge wa Upinzani walipokuwa wanatoka nje ya ukumbi wa Bunge huku wakizomewa na wenzao wa  CCM.

Wabunge hao wa upinzani walitoka nje muda mfupi baada ya Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson kuanza kuongoza kikao cha Bunge, ikiwa ni sehemu ya maazimio yao ya kuonesha kutokuwa na imani naye.

Hata hivyo, tuhuma za tukio hilo zilitua kwa Naibu Spika, lakini alieleza kuwa haweza kulitolea uamuzi suala hilo kwani hakumuona Mbilinyi akifanya kitendo hicho, lakini aliahidi kufuatilia mkanda wa video ya siku kikao hicho ili kujiridhisha.

 

Hesabu Za Antonio Conte Zashabihiana Na Kwadwo Asamoah
PSG Wahamishia Nguvu Zao Kwa Robin van Persie