Baada ya kupoteza mchezo wa mzunguuko wa tatu wa Kundi J, wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Benin, kikosi cha Taifa Stars kitaondoka jijini Dar es salaam leo Ijumaa (Oktoba 08) majira ya mchana Mchana kuelekea mjini Cotonou.

Stars itaondoka kwa usafiri maalum wa Ndege ya kukodi ya Shirika la Ndege la Tanzania ‘Air Tanzania’, huku ikiwa na matumaini ya kulipiza kisasi cha kufungwa bao 1-0 dhidi ya Benin jijini Dar es salaam jana Alkhamis (Oktoba 07).

Kocha Mkuu wa Stars, Kim Poulsen amesema wanatambua mchezo wa mzunguuko wa nne wa Kundi J dhidi ya Benin utakaochezwa Jumapili (Oktoba 10) utakuwa mgumu, lakini watapambana hadi dakika ya mwisho, ili kutimiza lengo la kuondoka la alama tatu ugenini.

“Tulishindwa kutumia nafasi ambazo tumezipata hivyo kwa ajili ya mchezo wetu ujao tutapambana kufanya vizuri na kupata pointi tatu muhimu.” amesema Kocha huyo kutoka nchini Denmark.

Baada ya michezo ya Jana Alkhamis (Oktoba 07), Msiammo wa Kundi J unaonesha Benin inaongoza ikiwa na alama alama 7, ikifuatiwa na DR Congo yenye alama 5 huku Tanzania ikiwa nafasi ya tatu na alama zake 4 na Madagascar inaburuza mkia, baada ya kupoteza michezo yote mitatu.

Majaliwa amsimamisha kazi Afisa Mipango Liwale
Sakho hatarini kuikosa Jwaneng Galaxy