Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI, imekanusha taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuhusisha Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Festo Dugange kuwa amejiuzulu ili kupisha uchunguzi.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano – TAMISEMI, Nteghenjwa Hosseah imesema taarifa za Naibu Waziri kujiuzulu ni uzushi na Wananchi wanaombwa kuipuuza kwani Dkt. Dugange bado ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Mbunge wa Jimbo la Wang’ingombe Mkoani Njombe.

Aidha, taarifa hiyo imezidi kueleza kuwa kwa sasa Dkt. Dugange bado anaendelea kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamini Mkapa iliyoko Jijini Dodoma.

Waziri huyo, alipata ajali ya gari usiku wa April 26,2023 na hivi karibuni viongozi kadhaa akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango kwa nyakati tofauti walimtembelea ili kujuklia hali yake.”

Waziri Mkuu mstaafu afikishwa Mahakamani kwa utajiri haramu
Apata Utajiri kwa Kucheza Aviator ya Meridianbet