Tanzania imetakiwa kulipa kipaumbele suala la chakula mashuleni kama sehemu ya juhudi za kupunguza umaskini na kuimarisha afya za watoto ambao ni nusu ya watu maskini duniani.

Ushauri huo umetolewa na Mkuu Shirika la Mipango ya Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Achim Steiner jijini New York nchini Marekani wakati akitoa ripoti ya hali ya umaskini duniani inayoonyesha kuwa nusu ya watu wanaoishi katika lindi la umaskini duniani wako chini ya umri wa miaka 18.

Amesema utafiti mpya umeangalia zaidi ya umaskini wa kipato ili kuona jinsi watu wanavyoathiriwa na umaskini kwa namna nyingine.

Aidha, utafiti huo umebaini jinsi watu wanavyoachwa nyuma katika mambo makuu matatu ambayo ni afya, elimu na utofauti wa maisha na kukosa mahitaji ya msingi kama maji, usafi, afya bora na elimu ya msingi.

Hata hivyo utafiti huo unaonyesha jinsi watu wanavyoendelea kuachwa nyuma katika maendeleo lakini kuna ushahidi wa msingi unaoonyesha kuwa mabadiliko yanaweza kutokea haraka kama ikitumika njia sahihi.

“Utafiti huo uliofanywa katika nchi 104 zenye uchumi wa chini na wa kati, watoto 662 wametajwa kuishi katika umaskini uliopindukia huku katika nchi 35 nusu ya watoto wote ni maskini,” amesema Steiner

Video: Ajali ya MV Nyerere mbunge alitabiri, Ni huzuni kubwa
Lukuvi apiga marufuku kampuni binafsi kupima ardhi