Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania – TMA, imetoa taarifa ya msimu wa kipupwe katika kipindi cha Juni hadi Agosti (JJA) 2023 ambacho kinatarajiwa kuwa na hali ya joto kiasi, baridi ya wastani katika maeneo mengi ya nchi.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Ladislaus Chang’a ameyasema hayo na kuongeza kuwa hali ya baridi ya wastani hadi joto kiasi, inatarajiwa kuwepo katika maeneo ya Nyanda za Juu Kusini -Magharibi pamoja na ukanda wa Ziwa Victoria huku vipindi vya baridi zaidi vinatarajiwa kujitokeza mwezi Juni.

Amesema, katika maeneo mengi ya Kanda ya Ziwa Victoria (Mikoa ya Mwanza, Mara, Geita, Kagera, Shinyanga na Simiyu) wanatarajia kuwepo kwa hali ya baridi ya wastani hadi joto la kiasi. ambapo kiwango cha joto la chini kinatarajiwa kuwa kati ya nyuzi joto 13 oC na 19 oC.

Kwa Ukanda wa Pwani ya Kaskazini (Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, maeneo ya kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba) Dkt. Chang’a amebainisha kuwa hali ya joto kiasi hadi baridi ya wastani inatarajiwa katika maeneo mengi.

Kwamba kiwango cha joto la chini kinatarajiwa kuwa kati ya nyuzi joto 22oC na 26oC kwa maeneo ya mwambao wa Pwani na visiwani na kati ya nyuzi joto 19oC na 22oC katika maeneo ya nchi kavu huku maeneno yenye miinuko yanatarajiwa kuwa na kiwango cha nyuzi joto chini ya 19oC.

Aidha ameongeza kuwa, kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara) hali ya joto kiasi hadi baridi ya wastani inatarajiwa katika maeneo mengi, kiwango hicho kinatarajiwa kuwa kati ya nyuzi joto 13 oC na 21 oC.

Chama afichua kilichoikwamisha Simba SC
Nasreddine Nabi afunguka mbinu za USM Alger