Utafiti uliofanywa na shirika la kimataifa la nguvu za atomiki (IAEA), kuanzia Machi 2019 hadi Aprili 2022, umegundua kuwa taratibu za kawaida za kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo zimepungua kwa asilimia 64 duniani kote.

Taarifa ya utafiti huo, imesema miaka miwili tangu shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni (WHO), kutangaza janga la COVID-19 wananchi wengi wanaohitaji huduma ya kupimwa magonjwa ya moyo ya wenye matatizo ya mishipa ya damu, wameendelea kupata tabu ya kuifikia huduma hiyo has katika nchi za kipato cha chini na cha kati.

Mkuu wa kitengo cha dawa za mionzi wa IAEA, Diana Paez amesema janga la Uviko-19 lilitatiza huduma ya afya ulimwenguni kote na kuathiri udhibiti wa magonjwa sugu kama matatizo ya moyo.

Madkatari wakiwa katika chumba cha upasuaji

“Hata hivyo urejeshaji wa huduma ya uchunguzi wa matatizo ya moyo ulitofautiana sana kurejeshwa kutoka maeneo mbalimbali duniani ambapo uliongezeka kwenye nchi za kipato cha juu na kuzidi kudorora kwenye nchi za kipato cha chini”. Amesema Paez.

WHO, imeorodhesha magonjwa ya moyo na mishipa ya damu kuwa inasababisha vifo vya watu milioni 18 kila mwaka na zaidi ya robo ya vifo hivyo hutokea katika nchi za kipato cha chini na cha kati.

Kauli ya Paez, pia imeungwa mkono na Daktari Andrew Einstein mtaalamu wa magonjwa ya moyo na mtafiti kutoka chuo kikuu cha Columbia kilichopo New York Marekani ambaye alishirikiana na Paez katika kuandika ripoti ya utafiti hizo.

Moyo

“Kupungua huku kwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo kuna uwezekano wa kusasabisha matokeo mabaya ya magonjwa ya moyo na mishipa ya damu katika nchi za kipato cha chini na cha kati kwa miaka ijayo na hivyo kuwa na ongezeko la utofauti wa afya ya moyo na mishipa duniani kote,” amesema.

Katika muendelezo wa awamu ya pili ya utafiti huo, wataalamu hao wameeleza kugundua matumizi ya vipimo vya mara kwa mara wakati wakisongeza mbele zaidi uchunguzi wao. Na kueleza watahitaji kuona ikiwa kupungua matumizi ya vipimo vya mkazo na ukuzaji wa hali ya picha za moyo unaendeleaje katika miaka ijayo.

“Ninaona kama haya ni maendeleo chanya, utumiaji mpana wa majalada ya picha pamoja na uboreshaji wa mbinu za majaribio za taswira. Hakuna kipimo kimoja kinachofaa kwa wagonjwa wote, badala yake tunajitahidi kutafuta kipimo sahihi kwa mgonjwa sahihi kwa wakati unaofaa,” amesema Dkt Einstein.

Vyakula vya mafuta

Utafiti huo, umeeleza kugundua matatizo ya kisaikolojia yaliyotokana na janga la Uviko-19, yaliwaathiri takriban asilimia 40 ya wafanyakazi na yaliathiri namna ya kuwatunza wagonjwa kwa asilimia 78 katika vituo vya kutolea huduma ya afya.

Viwango vya msongo wa mawazo vilikaribia kufanana katika makundi yote ya nchi za kipato cha juu na vile za kati na kipato cha chini, huku asilimia 38 ya madaktari katika nchi za kipato cha chini, na asilimia 37 katika nchi za kipato cha kati waliripoti kupata msongo wa mawazo wakati wa janga la Uviko-19.

Museveni na kauli tata kwa waganda
Serikali kusimamia miradi ya madini mkakati