Miili mingine 15 imepatikana katika msitu wa Shakahola, Pwani ya Kenya na kufanya idadi ya watu waliopatikana kufikia 226 wanaohusishwa na mchungaji tata Paul Mackenzie aliyewahimiza wafunge hadi wapoteze maisha ili wamwone Yesu.

Kufuatia sakata hilo, Serikali imetangaza marufuku ya watu kutembelea eneo hilo wakati huu ambapo inaendelea na msako zaidi ili kubaini makaburi ya watu waliofukiwa na kuwabaini wale ambao wapo hai ili kuwaokoa.

Hata hivyo, wenyeji wa eneo hilo wameungana kuwasaidia maafisa wa usalama kwa kuwakabidhi wafuasi wa mchungaji huyo wanaotorokea kijijini humo kwa maafisa wa polisi huku Mzee Taabu Kajole ambaye ni mjumbe wa kumi akisema wataendelea kutoa ushirikiano.

Serikali ya Kenya ilitangaza marufuku ya kusogelea eneo hilo kutokana na hali ya misukosuko na uhalifu baada ya mamia ya makaburi kupatikana kwenye shamba hilo.

Simba SC yasitisha usajili wa Mlinda Lango
Mbeya City kutia mchanga pilau la Ubingwa?