wakati baadhi ya mataifa ya Ulaya yakilegeza vizuizi vilivyowekwa ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona, Wahispania waliruhusiwa jana kutoka majumbani mwao na kuingia mitaani kwa mara ya kwanza baada ya kufungiwa ndani kwa siku 48.

Kuanzia  Madrid  hadi Mallorca, Wahispania  walimiminika  mitaani baada  ya  kuruhusiwa  kufanya  mazoezi na  kutembea  huru  nje baada  ya  serikali  kulegeza wiki  saba za  udhibiti  mkubwa.

nchi  hiyo ilikuwa  na  idadi  ya  juu  kabisa  ya  vifo vya wagonjwa wa covid 19, vilivyofikia zaidi  ya  25,000. 

 “Baada  ya  wiki  kadhaa za  kufungiwa, nilikuwa nahitaji  sana  kutembea  nje, kukimbia, na kuona dunia,” alisema mshauri  wa   masuala  ya  fedha Marcos Abeytua  mjini  Madrid alipoongea na DW.

Uhispania, Ujerumani, Austria na  mataifa  ya  Scandinavia taratibu yanalegeza  vikwazo vya  kuwazuwia  watu  kutoka  majumbani, wakati  kesi  za  virusi  vya  corona  zikipungua licha ya  kuwa  hatua za  watu  kukaa  mbali  mbali  zitaendelea, matumizi  ya barakoa pamoja  na  uchunguzi  kujaribu  kufuatilia  maambukizi.

Siku ya uhuru wa vyombo vya habari: EU wakemea vizuizi kipindi cha Corona
Mtoto auawa kwa kushambuliwa na fisi nyumbani