Mbunge wa jimbo la Kinondoni,  Maulid Mtulia (CUF) amewatia moyo wakazi wa Bonde la Msimbazi waliokumbwa na zoezi la bomoabomoa lililoendeshwa kwa awamu ya kwanza mwishoni mwa mwaka uliopita.

Akiwahutubia wakazi wa jimbo hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Magomeni Barafu, Mtuli aliwaambia wananchi hao kuwa baada ya kubaini kuwa agizo na utekelezaji wa agizo la bomoabomoa vilifanywa kimakosa, walifanya utaratibu wa kuishitaki Serikali Mahakamani ili kuhakikisha wananchi wanapata haki yao.

Alisema kuwa Mwanasheria Abubakar Salum ambaye ndiye mwenye jukumu la kusimamia kesi hiyo, ameshakamilisha taratibu hizo  na wanachosubiri ni kupangiwa tarehe ya kuanza kuskilizwa kesi hiyo, lengo likiwa kuhakikisha kuwa pamoja na mambo mengine, waathirika wa zoezi hilo wanalipwa fidia.

Aidha, alisema kuwa wakati wakisubiri maamuzi ya mahakama kupitia kesi hiyo, tayari waathirika wameandaliwa mpango wa kujikimu ili kunusuru hali yao kimaisha kutokana na kukosa makazi kupitia zoezi la bomoabomoa.

Mwishoni mwa mwaka uliopita, Serikali iliendesha zoezi la bomoabomoa kuwaondoa watu walijenga katika maeneo yaliyoko mabondeni, maeneo ya wazi kinyume cha sheria ya mazingira.

 

Mkuu wa Wilaya amtaka Waziri Nchemba kutokanyaga kijijini kwake
Kituko: Msanii mkubwa wa Afrika Kusini adai Beyonce ni Mwanae, asimulia alivyomgawa (video)