Uongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) umezungumzia kasi aliyoanza nayo rais John Magufuli hususan katika kupambana na ufisadi na uzembe kazini.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu amesema kuwa anachokifanya Magufuli anatekeleza ilani ya uchaguzi ya chadema.

Ameeleza kuwa wakati wa kampeni, Chadema walieleza namna watakavyopambana na ufisadi, kuwa na utaratibu bora wa utendaji kazini na kutokomeza uzembe kwa watumishi wa umma na kwamba mambo hayo yanatekelezwa na Dk. Magufuli.

Naibu Katibu Mkuu huyo wa Chadema alisema kuwa Dk. Magufuli atakutana na changamoto kwa kuwa mambo anayoyafanya sasa hayakuwa kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

“Akiomba ushauri tunatoa kwa maana namna gani atekeleze, lakini ni mapema mno kusema kama ana dhamira ya kufanya. Pengine anayafanya kwa ajili ya kujitafutia umaarufu wa haraka haraka,” Mwalimu aliliambia gazeti la Mwananchi.

Ripoti: Bilionea wa ‘Unga’, El Chapo alifanya Mapenzi Gerezani Mara 46 kabla ya kutoroka
Ripoti: Mawaziri wa JK watajwa kuhusika Ufisadi wa Mabilioni