Bingwa wa dunia wa riadha, Mjamaica Usain Bolt amepata watoto mapacha wa kiume ambao amewaweka wazi kupitia mtandao wa Instagram akisherehekea Siku ya Baba Duniani.

Bolt amepata zawadi hiyo ya mapacha kutoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia kwa mkewe Kasi Bennett. Kupitia picha aliyoweka mtandaoni inaonesha akiwa na mpenzi wake huyo, binti yao Olympia na mapacha wao.

Watoto hao waliopewa majina ya Thunder na Saint Leo hawakuelezewa wamezaliwa siku gani. Dada yao Olympia Lightning yeye alizaliwa mwaka jana.

Bolt alistaafu riadha mwaka 2017 akiweka rekodi ya kuwa binadamu anayeenda kasi zaidi. Hivyo, hatashiriki kwenye mashindano yam waka huu ya Olympic yanayofanyika Tokyo, Japan. Aliweka rekodi ya kutumia sekunde 9.58 kukimbia umbali wa mita 100 katika michuano ya ubingwa wa dunia ya Berlin ya mwaka 2009.

Mwanariadha huyo mstaafu ambaye amekuwa Bingwa wa Dunia mara 11, ameiambia CNN kuwa anapanga kushiriki kama shabiki na sio mshindani tena.

on Day 9 of the Rio 2016 Olympic Games at the Olympic Stadium on August 14, 2016 in Rio de Janeiro, Brazil.

“Sijawahi kupata fursa ya kuangalia michuano ya Olympic, iwe ni kuogelea, mpira wa miguu au hata kukaa tu na kuangalia michezo yote. Kwahiyo nina furaha sana kupata nafasi ya kushuhudia michuano ya Olympic kama shabiki wa kweli,” amesema Bolt.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Juni 22, 2021
Mkutano Baraza la Mawaziri EAC waanza, EACO sasa kurasimishwa