Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba amesema wanatarajia kutumia shilingi 575,000,000 kwa ajili ya mradi wa Kupeleka vifaa maalum vya TEHAMA kwa ajili ya kujifunzia kwa Shule 16 zenye watoto wa mahitaji maalum hapa nchini.

Mashiba ameyasema hayo leo hii leo Februari 13, 2023 Jijini Dodoma wakati akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mfuko huo mbele ya waandishi wa habari na kuongeza kuwa vifaa vitakavyopelekwa katika shule hizo ni pamoja na na TV, Braille Machine (Nukta Nundu), Orbit reader (Machine za Kisasa), Laptops, na Embosser (Printa ya nukta nundu).

Amesema, Shule zitakazonufaika ni pamoja na Sekondari ya Mpwapwa (Dodoma), Sekondari ya Mkolani (Mwanza), Sekondari ya Kashaulili (Mpanda-Katavi), Sekondari ya Morogoro (Morogoro), Sekondari ya Shinyanga (Kishapu-Shinyanga), Sekondari ya Wavulana Songea (Songea), Sekondari ya Kazima (Tabora) na Sekondari ya Haile Selassie (Mjini Magharibi – Zanzibar).

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba.

Mashimba ameongeza kuwa, “shule hizi 16 zitanufaika na naamini vifaa hivi vitakapowafikia hawa watoto wenye mahitaji maalum vitawasaidia katika kujifunza na kufikia malengo na nia ya mfuko wa UCSAF ni kuhakikisha nchi nzima inaunganishwa na mawasiliano.”

Aidha, amesema kuwa jumla ya shule 811 zimefikishiwa vifaa vya TEHAMA ambapo kwa wastani kila shule imepewa Kompyuta 5, Printa 1 na Projekta 1 na kwa mwaka wa fedha wa 2022/23, Shule 150 zitafikishiwa vifaa vya TEHAMA, bajeti yake ikiwa ni TZS 1,950,000,000/- na vifaa hivyo vitasaidia wanafunzi kusoma katika shule hizo 811.

Akizungumzia hali ya mawasiliano nchini, Mashiba amesema mwaka 2009 huduma za Simu ilikuwa asilimia 45 wakati kwa sasa imeongezeka hadi kufikia asilimia 96, teknolojia ya 2G coverage yake asilimia 96, 3G asilimia 72, 4G asilimia 55 na Geographical Coverage ya 2G asilimia 69, 3G asilimia 55 na 4G ni asilimia 36.

Kwa upande wa Ujenzi wa Minara Vijijini, Mtendaji huyo amesema UCSAF imeingia mikataba kufikisha huduma katika kata 1,242 zenye vijiji 3,654, Wakazi 15,130,250 ambapo Minara 1,087 yenye vijiji 3,378 na wakazi 13,320,750 na Utekelezaji unaendelea katika Minara 155 yenye vijiji 276 na wakazi 1,809,500 kwa ruzuku iliyotolewa yaTZS bilioni 199 ikiwemo pia Mradi wa kimkakati wa Zanzibar, Minara 42, Shehia 38 ruzuku TZS bilioni 6.9.

Mstaafu atishia kujinyonga kwa kulipwa milioni 45
Jaribio ajali ya Ndege Kahama lazua Taharuki