Uturuki imegoma kufuata maagizo ya Urusi kuomba radhi kwa kuidungua ndege ya kijeshi ya nchi hiyo.

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan amesema kuwa kamwe nchi yake haitaomba radhi kwa kuidungua ndege hiyo ya Urusi kwa kuwa ilichofanya sio tu kwamba ni haki yake bali ilikuwa jukumu la nchi hiyo kulinda anga lake.

Erdogan alisisitiza kuwa ndege ya Urusi ilivunja sheria na kupita kwenye anga lake huku ikipuuzia ishara za tahadhari zilizotolewa ndani ya dakika 10.

“Hakuna waziri Mkuu au waziri yeyote wa Uturuki atakayeomba radhi kwa tukio la kuiangusha ndege ya Urusi,” aliseam rais Erdogan.

Awali, Urusi iliitaka Uturuki kuomba radhi kwa kuangusha ndege yake kwa madai kuwa haikugusa anga la nchi hiyo bali iliangushwa ikiwa katika anga ya Syria ilikokuwa ikiwasaka wapiganaji wa kundi la IS.

Hata hivyo, rais wa Uturuki alipinga madai ya Urusi na kueleza kuwa hakuna wapiganaji wa Urusi katika eneo hilo bali wapo ndugu na jamaa wa Uturuki hivyo yeyote anayeshambulia eneo hilo anawaangamiza Waturuki.

Posho Za Wabunge Zapigwa Chini
Burna boy Aponda Tuzo Za Nigeria, Adai Zimejaa Siasa