Kiungo mkabaji kutoka nchini Brazil Fábio Henrique Tavares “Fabinho” amependekezwa kuwa mbadala wa beki Virgil van Dijk, ambaye atakua nje ya kikosi cha Liverpool, kwa kipindi chote cha msimu kilichosalia.

Van Dijk aliumizwa na kipa wa Everton, Jordan Pickford wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya England Jumamosi iliyopita na hivyo anahitaji kufanyiwa upasuaji, jambo linalomweka kwenye hatari ya kushindwa kurudi tena uwanjani ndani ya msimu huu.

Jambo hilo linamfanya meneja wa Liverpool Jurgen Klopp kuwa na wakati mgumu wa kupanga mbinu mbadala, ambazo zitamuwezesha kuziba pengo la beki huyo kutoka nchini Uholanzi.

Hata hivyo Van Dijk amempunguzia mawazo meneja huyo kutoka nchini Ujerumani kwa kumpendeza kiungo Fabinho, kwa kusema anafaa kuwa chaguo sahihi la kuziba nafasi aliyoiacha wazi.

“Ninaamini Fabinho ana uwezo mkubwa wa kuziba pengo langu, kwa kuwa ana ubora wa kutosha kwa kipindi hiki ambacho nitakosekana uwanjani kwa muda mrefu kutokana na kuumia.” Amesema Virgil van Dijk.

Fabinho aliwahi kucheza nafasi ya beki sambamba na Van Dijk katika mchezo dhidi ya Chelsea mwanzoni mwa msimu huu, ambapo aliweza kumdhibiti mshambuliaji Timo Werner na hakufurukuta.

Na Van Dijk alimsifia Fabinho na kusema mchezaji huyo ana uwezo mkubwa wa kucheza beki wa kati. “Bora kabisa,” alisema Van Dijk akizungumza kiwango cha Fabinho dhidi ya Chelsea.

“Nilimwambia na nadhani alikuwa mchezaji bora wa mechi. Kumdhibiti mshambuliaji kama Timo Werner na asifunge sio kazi nyepesi.”

Kaijage: Jukumu lakutangaza matokeo ni la Tume ya Uchaguzi
Simba SC: Tupo tayari kuwavaa Tanzania Prisons