Siku chache baada ya Rais, John  Pombe Magufuli kutembelea wananchi wa Magomeni Kota ambao walikuwa wameondolewa katika makazi yao kwa ahadi ambazo hawakutekelezewa kwa miaka mingi, neema imeanza kuonekana baada ya ahadi ya Rais Magufuli ya kuwajengea nyumba wakazi hao kuanza.

Taarifa za kuanza kwa ujenzi huo zimetolewa leo Oktoba 8, 2016 na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Elius Mwakalinga wakati akuhutubia katika mkutano wa maombi yaliyoandaliwa na wakazi wa Magomeni Kota kwaaajili ya kumuombea Rais Magufuli na Serikali kwa ujumla.

Mwakalinga amewahakikishia wakazi waeneo hilo kuwa hatua za awali tayari zimeanza na ujenzi huo utakamilika ndani ya miezi kumi. Bofya hapa kutazama video

Video: 'Rais Magufuli ni mtanzania wa pekee sana' - DC Hapi
DC Ndejembi akifungia chuo cha ualimu Nkuruma-mkoka