Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amewashukuru wakazi wa Magomeni Kota kwa kuandaa mkutano wa maombi ya kumwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania, Dk.  John Pombe Magufuli.

Akihutubia katika mkutano huo leo Oktoba 8, 2016, Hapi amesema Rais Magufuli mbali na kuwa mtanzania pia ni mtu wa pekee sana na aliyesubiriwa kwa muda mrefu, hivyo amewataka wakazi hao pamoja na wananchi wote kwa ujumla kuendelea kumuombea Rais Magufuli

Hapi amesema kazi za Rais Magufuli zinaonekana ambapo ahadi aliyowaahidi wakazi hao ya kuwajengea nyumba baada ya kutolewa katika makazi yao imeanza kuonekana kutimia, na tayari wakazi hao wametangaziwa fursa kufuatia ujenzi huo. Bofya hapa kuazama video

Mbunge wa Chalinze Akabidhi Magodoro 200 Shule ya Sekondari Moreto
Video: Ahadi ya JPM kwa wananchi wa Magomeni Kota kuanza.