Rapa Cardi B amefunguka kuhusu tetesi zilizokuwa zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa wasanii wengi wakubwa ikiwa ni pamoja na Rihanna, wamemu-unfollow kufuatia tukio lake la kumshambulia Nicki Minaj kwa viatu.

Taarifa zilizokuwa zimesambaa mitandaoni zinaeleza kuwa huenda Cardi B akapata wakati mgumu wa kufanya kazi na baadhi ya wasanii ambao wameonesha kukerwa na kitendo cha kutaka kufanya vurugu dhidi ya Nicki Minaj kwenye tamasha la mitindo wiki kadhaa zilizopita, kwani wameamua kutojihusisha naye hata kwenye mitandao ya kijamii.

Rapa huyo wa kike ametumia Instagram Live kuzungumza na mashabiki wake wiki hii, ambapo amekanusha na kueleza kuwa wengi waliotajwa kwenye tetesi hizo ikiwa ni pamoja na Rihanna kuwa wamemu-unfollow hata hawajawahi kum-follow.

“Hao mastaa hawakuwahi hata kunifuata [Instagram]. Kwanini hamkomi kutengeneza tetesi kujaribu kuonesha kuwa wakati wangu umekwisha?” Alihoji.

“Wakati wangu ukifika kikomo, mtaona dhahiri kwamba wakati wangu umekwisha,” aliongeza.

Cardi B alijikuta akifyatuka na kuanzisha ugomvi wa ‘ngumi’ na Nicki Minaj kwenye tamasha la mitindo la ‘New York Fashion Week’ akifikia hatua ya kumrushia viatu mkali wa ‘Barbie Thing’.

Hata hivyo, viatu hivyo havikumpata Nicki huku Cardi akiambulia nundu usoni kutokana na purukushani kati yake na walinzi.

Kinachofurahisha, Cardi B na Nicki Minaj walihudhuria tena kwa pamoja tamasha la mitindo la ‘Milan Fashion Week’ wikendi iliyopita, lakini amani ilitawala kati yao.

TCU yafuta vyuo lukuki
Mtoto aliyepotea apatikana polisi