Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Simon Sirro amesema kuwa jeshi hilo limekusanya shilingi milioni 304 ndani ya siku tatu kwa makosa mbalimbali ya uvunjaji sheria za barabarani.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Sirro ametaja idadi ya magari yalikamatwa kuwa ni 9,127, pikipiki 498, dala 3,839 na magari binafsi5,288.

Amesema kuwa watumiaji wa vyombo hivyo vya moto walikamatwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kutokuvaa helmet na kupakia mishikaki kwa waendesha bodaboda, makosa ya uchepukaji kwa daladala na watu binafsi.

“Ndani ya siku tatu tumeweza kukusanya milioni 304.590,000/= kwa makosa mbalimbali ya barabarani, hivyo nawaasa watumiaji wa barabara kuwa makini,”amesema Sirro.

Video: Mtoto asimulia jinsi alivyowaokoa wenzake 9 kuzama ziwa victoria
Video: Watu 4 waliopasua maiti kutoa dawa za kulevya wakamatwa