Mbunge wa Jimbo la Mwibara Mkoani Mara, Kangi Lugola amesema kuwa Serikali inatakiwa kuongeza maslahi ya askari polisi ili kuwawezesha kufanya kazi kwa weledi na umakini.

Ameyasema hayo mapema hii leo Bungeni mjini Dodoma alipokuwa akichangia hoja katika bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani.

Amesema kuwa askari polisi wanafanya kazi kubwa na ngumu hivyo maslahi yao yanatakiwa kuwa ya kuridhisha kuweza kuhudumia familia zao na wao wenyewe wakiwa kazini.

“Mwenyekiti naongea kwa uchungu kwa sanbabu hata mimi nimepitia huko, najua kila kitu kwani hata Waziri hapa anchokiongea ni maneno tu, lakini sidhani kama kuna utekelezaji wowote,”amesema Lugola

?Live: Yanayojiri Bungeni uchaguzi wa wabunge wa Chadema EALA
Wananchi Pwani washauriwa kushirikiana katika masuala ya kijamii