Koffi Olomide ambaye ametua nchini Kenya leo asubuhi kwa ajili ya kufanya tamasha kubwa linayosubiriwa kwa hamu na mashabiki, amejikuta akighafirika katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta na kumtwanga teke mnenguaji wake wa kike.

Video iliyonaswa na kamera za waandishi wa habari waliofika katika uwanja huo kushuhudia mapokezi ya mwimbaji huyo na bendi yake, inamuonesha akimrushia teke mnenguaji huyo na kujaribu kumfuata ili amuadhibu zaidi kabla ya kuzuiwa na maafisa wa polisi waliokuwa karibu naye.

Chanzo cha tukio hilo inadaiwa kuwa mnenguaji huyo alinekana kumtolea maneno mabovu mke wa Koffi ambaye pia ni mwimbaji wa bendi hiyo, Cindy Le Couer.

Ikumbukwe kuwa Koffi ni moja kati ya watu wasioruhusiwa kabisa (strictly) kumshambulia mtu bila sababu za kujihami kwani ni mtaalam wa mapigano ya ‘Martial Art’ akiwa na mkanda maalum (Black Belt) aliupata miaka mingi iliyopita.

Kipre Tchetche Akaribia Kuondoka Azam Complex
Katibu Mkuu Wizara Ya Elimu Awataka (TCU) Na (NACTE) Kufuta Programu Kwa Vyuo Visivyosajiliwa