Majonzi yatawala Ukonga majumba sita, baada ya kijana aliyekuwa anaishi kwa kupumlia mashine kufariki jana jioni, akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya Mloganzila.

Kijana Hamad Awadh (28), aliishi kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja akiwa na matatizo katika njia ya upumuaji.

Dar 24 ilifika nyumbani kwake mwezi Agosti mwaka huu ili kumsaidia kupata msaada kutoka kwa wasamalia wema wa fedha za matibabu na wiki kadhaa baadaye alifanikiwa kupata na kuanza kupatiwa matibabu Muhimbili.

Siku ya Alhamisi majira ya saa kumi jioni alifariki, ndugu zake wameeleza jinsi walivyoishi naye enzi za uhai wake, na jinsi alivyokiona kifo chake,…Bofya hapa kutazama.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 19, 2019
Video: Wazazi wanaowashawishi watoto wao kufanya vibaya kwenye mitihani kushitakiwa