Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kuwauwa majambazi watano katika operesheni maalum iliyofanyika ya kuhakikisha usalama unapatikana wakati wote kwa raia.

Hayo yamesmwa na Kamishna wa Polisi Kamanda, Lazaro Mambosasa hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa mara baada ya majambazi kuona wanafuatiliwa na askari walianza kuwarushia risasi, kitendo ambacho kiliwafanya askari hao kujibu mapigo na kufanikiwa kuwaua majambazi hao.

Amesema kuwa baada ya kufanya upekuzi walikuta mabomu saba ya kurusha kwa mkono, pikipiki moja, na silaha aina ya SMG moja na Magazine moja ambayo ilikuwa na risasi kumi na sita.

“Niseme tu kuwa juhudi za kuutambua mtandao huo unafanywa ili kuweza kubaini na kuutokomeza kwani ni hatari kwa raia na mali zao,”amesma Kamanda Mambosasa

Habari picha, Luhaga Mpina akiteta jambo na watumishi
Video: ACT- Wazalendo wazungumzia mwanachama wao kujiengua