Paris Saint-Germain imeibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya klabu ya Bayern Munich katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya uliopigwa usiku wa jana katika uwanja wa Parc des Princes.

Dakika mbili baada ya mchezo huo kuanza beki wa kulia mbrazili Dani Alves aliipatia PSG bao la kuongoza kabla ya Edinson Cavani kupachika bao la pili dakika ya 31 na Neymar kufunga bao la tatu dakika ya 63.

Mchezo huo ulitarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na ubora wa vikosi vya timu zote mbili lakini Bayern Munich yenye historia kubwa katika michuano hiyo ilijikuta ikikubali kipigo cha 3-0.

Tazama mabao ya mchozo huo hapa chini.

Chadema wamgomea Mwigulu
Hasheem Thabeet ajiunga na ligi ya kikapu Japan