Maadhimisho ya siku ya mazingira duniani kitaifa yanatarajiwa kufanyika Julai 5 mwaka huu Butiama Mkoani Mara huku kukitarajiwa kuwa na mijadala mbalimbali itakayojadiliwa kuhusu utunzaji wa mazingira.

Hayo yamesemwa mapema hii leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Janury Makamba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa maadhimisho hayo yatafanyika Butiama ili kuenzi mchango wa Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika utunzaji mazingira, ambapo enzi za uhai wake alisisitiza umuhimu wa mazingira.                                                                                                                      

JPM amteua Sirro kuwa Mkuu wa Polisi (IGP)
JKT waibuka kidedea mashindano ya ngumi