Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli jana amewaapisha Wakurugenzi wa Miji, Manispaa na Halmashauri za Wilaya.

Rais Magufuli amewataka wawe ni watatuzi wa kero za wananchi badala ya kuwa watengeneza kero na akasisitiza wawe mitume wazuri kwa wananchi.

“Kaondoeni kero kwa wananchi wa hali ya chini, wako huko wanatozwa kodi ndogondogo hata za kuuza mchicha tu. Mtu akivuna mpunga wa kula nyumbani kwake pia anatozwa kodi, ni lazima kodi hizi mkazizuie kwa sababu tuliahidi kupunguza kero kwa wananchi na siyo kuongeza kero kwao, – Rais Magufuli

Mahakama yawarudisha kizimbani Wasira, Esther Bulaya kugombea ubunge
Msami Afungukia Uhusiano wake na Kajala