Taasisi ya Chakula na Lishe nchini, TFNC katika maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji imesema kuna baadhi ya kina baba wana tabia ya kunyonya maziwa ya kinamama wakati wa kunyonyesha wakiamini kuwa maziwa hayo yana virutubisho vinavyoongeza nguvu za kiume.

Akizungumza na Dar24, Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, TFNC Gelagista Gwarasa amesema hakuna tafiti zinazoonyesha ukweli juu ya suala hilo japokuwa maziwa ya mama yana virutubisho vyenye uwezo wa kuongeza nguvu za kiume.

Aidha ameonya tabia hiyo ya kinababa kunyonya maziwa ya mama akisema kuwa zipo aina nyingi ya vyakula ambavyo huongeza nguvu za kiume, amewaasa wanaume kuwaachia watoto maziwa wanyonye ili waweze kutosheka na kupata virutubisho vyote vya muhimu katika kujenga miili yao kiakili na kimwili.

Tazama video hapa chini.

LIVE SIMIYU: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Katika Sherehe na Maonyesho ya Nane Nane
Video: Lissu atua mahakamani kupigania ubunge wake, Siku 10 SADC kujaza Watanzania bil 4