Bodi ya Udhamini ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), chini ya uenyekiti wa Profesa Samwel Wangwe imewasimamisha kazi watumishi 12 wa shirika hilo kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma, matumizi mabaya ya ofisi, kukiuka sheria na kanununi za usimamizi wa miradi na manunuzi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, waliosimamishwa na Bodi hiyo ni pamoja na wakurugenzi sita, mameneja watano na mhasibu mmoja. Imeelezwa kuwa watumishi hao wamesimamishwa ili kupisha uchunguzi.

Imewataja waliosimamishwa na nafasi zao kwenye mabano kuwa ni Yacoub Kidula (Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi), Ludovick Mrosso (Mkurugenzi wa Fedha), Chiku Matessa (Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala), Sadi Shamliwa (Mkurugenzi wa Udhibiti Majanga), Pauline Mtunda (Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Hesabu za Ndani) na Crescentius Magori (Mkurugenzi wa Uendeshaji).

Kadhalika, Mameneja waliotumbuliwa ni Amina Abdallah (Meneja Utawala), Abdallah Mseli (Meneja Uwekezaji), Mhandisi John Msemo (Meneja wa Miradi), Chedrick Komba (Meneja Kiongozi –Mkoa wa ki-NSSF wa Temeke), Mhandisi John Ndazi (Meneja Miradi). Pia, Mhasibu Mkuu wa Shirika hilo, Davis Kalanje amekumbwa na uamuzi huo wa Bodi.

Bodi hiyo ya Udhamini ya NSSF ilifikia uamuzi huo katika kikao chake kilichofanyika Julai 15 mwaka huu.

CCM yapeleka neema Dodoma, yashika hotel 306, Kinana ang’atuka
Mpango Wa Serikali Kubadili Vyuo Vya Ufundi kuwa Vyuo Vikuu Wakwama