Serikali nchini, imetakiwa kutilia mkazo ujenzi wa vyumba maalum vya kujisitili wanafunzi wanapopatwa na hedhi, kutokana na miundombinu iliyopo kutokuwa rafiki na hivyo baadhi yao kukosa masomo.
Wakiongea kwa nyakati tofauti, baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngerengere iliyopo Wilaya ya Morogoro wamesema wamekuwa wakipoteza muda mwingi wa masomo ili kuweza kupata suluhu ya kujisitiri wakati wa kipindi cha hedhi.
“Upatikanaji wa Taulo za kike pia ni wa shida, miundombinu pia ni suala linalo tutatiza asilimia kubwa tulazimika kusalia nyumbani kipindi chote
cha hedhi,” walisema.
Hata hivyo, uongozi wa shule hiyo umesema umekuwa ukifanya jitihada za kukabiliana na hali hiyo na kuhakikisha angalau taulo za akiba zinakuwepo, kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi kujisitili inapotokea kwa dharula.
Hata hivyo, tayari Kampuni ya Softcare ikiongozwa na mwakilishi wake, Lucy Msami waliifikia shule hiyo ya Ngerengere kuwawezesha wanafunzi 480 kupata taulo za kike za kuwasitiri wakati wa dharula, mahindi kilo 500 na maharage kilo 200 za akiba ya chakula.