Timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 20, Tanzanite imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jana.

katika mechi hiyo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia zitakazofanyika Costa Rica na Panama kuanzia Julai 2-22 mwaka huu, hadi kipindi cha kwanza kinakamilika hakuna timu iliyokuwa imefanikiwa kugusa nyavu ya mwenzake.

Katika kipindi cha pili ambacho kilianza kwa kasi, Uganda ilianza kwa kupata bao la kuongoza kupitia kwa Nalukenge Juliet dakika ya 47, lakini Tanzania wakafanikiwa kusawazisha katika dakika ya 58 kupitia kwa Diana Lucas aliyemalizia pasi ya Asha Mashaka.

Uzembe wa mabeki wa Uganda dakika ya 68 uliwapa zawadi ya kona Tanzania iliyopigwa na Diana Lucas na kuzamishwa kimiani na Opah Clement.

Kwa sasa Timu ya Tanzania itahitaji sare au ushindi wowote katika mechi ya marudio inayotarajiwa kuchezwa Februari Mosi mwaka huu nchini Uganda ili kusonga mbele.

Rukwa: Hofu yazidi, wazazi wawapa watoto dawa za kupanga uzazi
Ajinyonga baada ya mkewe kuuza kondoo

Comments

comments