Mkuu wa mkoa wa Lindi, Zainab Telack amewataka wazazi kuwapatia watoto nafasi ya kushiriki kikamilifu katika masomo, ili waweze kutimiza ndoto zao.

Telack ameyasema hayo mara baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kukagua ujenzi wa jengo la utawala shule ya Sekondari ya Wasichana Ruangwa, pamoja na madarasa katika Shule ya Sekondari ya Kitandi wilayani Ruangwa.

Amesema, “Jitahidini kufanya vizuri kitaaluma, mjitambue nyie ni wanafunzi na hivyo mjiepushe na vishawishi vyovyote vitakavyokwamisha maendeleo yenu kitaaluma. Wananchi tuwalinde watoto wetu ili watimize ndoto zao. Mtoto wa mwenzio ni wako.”

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack akiongozana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati wa ukaguzi wa Mradi wa Ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondary Mary.

Akiwa katika shule hiyo, Waziri Mkuu amewataka wananchi kuacha kuvamia maeneo ya karibu kwa kuwa Serikali imeyahifadhi kwa ajili matumizi ya baadae ya taasisi husika. “Hapa palikuwa pori hapakuwa na shamba pasiguswe.”

Aidha, pia Majaliwa alikagua ujenzi wa madarasa ya ghorofa yanayojengwa katika shule ya msingi Likangara, na kuupongeza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa kwa ubunifu wa mradi huo unaohusisha vyumba nane vya madarasa, matundu 24 ya vyoo na ofisini nne.

Hassan Dalali amng'ata sikio Mangungu
Dube afichua siri ya kuiadhibu Simba SC