Wasanii maarufu USA wanafanya kampeni ya kununua bidhaa zote katika duka la nguo la Marathon la marehemu Nipsey Hussle kama njia ya kusaidia familia yake.

Meek Mill, The Game, T.I, 2Chainz, J.R Smith na DeMar DeRozan kutoka NBA tayari wamenunua T-Shirts, masweta na kofia.

Nipsey Hussle alikuwa rapa wa Marekani mwenye asili ya Eritrea, baba yake ni raia wa Eritrea aliyeingia Marekani akikwepa vita iliyokuwa ikiendelea nchini kwake.

Aliuawa Machi 31 na kuzikwa Aprili 11, 2019. Wiki hii, albam yake ya ‘Victory Lap’ ilirejea tena kwenye chart za Billboard 200. Albam hiyo ilikuwa miongoni mwa albam zilizowania tuzo za Grammy mwaka huu katika kipengele cha Albam Bora ya Rap, lakini bahati ilimuangukia Cardi B na ‘Invasion of Privacy’.

Nipsey Hussle ambaye ameagwa rasmi na mamilioni ya watu duniani kote, aliuawa kwa kupigwa risasi sita akiwa nje ya duka lake la Marathon katika viunga vya Los Angeles.

 

Mabasi ya mwendokasi 70 yashikiliwa TRA
Rais TFF aihofia Senegal, asema hana shaka na Algeria, Kenya

Comments

comments