Hatimaye washtakiwa watano wa waliotajwa kuhusika katika ubadhilifu wa fedha katika akaunti ya External Payment Arrears (EPA), wameachiwa huru na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Jopo la mahakimu lililosikiliza kesi hiyo, jana limesoma hukumu ya kesi hiyo na kueleza kuwa watuhumiwa wameachiwa huru baada ya upande wa Jamhuri uliokuwa unawashtaki watu hao kushindwa kuthibitisha pasipo na shaka yoyote.

Washitakiwa hao walitajwa kuwa ni Rajabu Maramba, Ajay Soman, Jay Soman, Imani Mwakosya, Esther Komu na Bosco Kimela, walikuwa wakikabiliwa na kosa la kula njama na wizi wa Shilingi bilioni 5.9 katika akaunti ya EPA iliyokuwa katika Bank Kuu ya Tanzania.

De Bruyne Ampeleka Draxler VfL Wolfsburg
Mbokani Kucheza Soka England 2015-16