Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezungumza na wafanyabiashara wa Soko la Kimataifa la Kariakoo katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam ambao wengi wao wanatoa changamoto zao hasa suala la ushuru wa Bandari ambao unawakandamiza.
Akiwa katika maongezi hayo, Majaliwa aliwataka wafanyabiashara hao kuongea kwa uwazi changamoto zinazowakabili hata kama ikimaanisha kumkosoa yeye, akisisitiza kwamba hakuna atakayedhurika kwa atakachokisema.
Aidha, wengi wa wafanyabiashara hao wamesema Viongozi wa Serikali na hasa watunga sera wamekuwa hawawashirikishi wadau katika kuchukua maoni yao hali inayofanya kukadiria wanachokifikiria wakati ni tofauti na uhalisia wa mtaani.
Wamemuomba Waziri Mkuu kufanyia kazi kero zao na kusema ulipaji kodi unawezekana lakini mfumo uliopo haina mashiko kwani unadhohofisha uchumi wa nchi na pato la mtu mmoja mmoja kitu ambacho hakina tija.