Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ummy Mwalimu amemtaka Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Ashraf Bige kujitathmini kwakukubali kuwa ameridhishwa na Ujenzi licha ya kuwepo kwa mapungufu katika ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo.

Akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe leo Waziri Ummy amesema ameridhishwa na Maendeleo ya ujenzi wa Hospitali hiyo lakini Halmashauri ihakikishe inasimamia mapungufu yaliojitokeza na kuhakikisha wanakamilisha ujenzi kwa wakati

Waziri Ummy amesema kuwa hajaridhishwa na utendaji kazi wa muhandisi huyo kwa kuwa hajatimiza wajibu wake kikamilifu katika usimamizi wa ujenzi wa Hospitali hiyo kwa kuwa kumekuwepo na mapungufu mengi katika ujenzi huo


“Haiwezekani milango ikatofautiana na kusababisha muonekano wa jengo kuwa mbaya halafu Mhandisi anasema ameridhishwa na Ujenzi, na kuagiza ujitathmini kama anatosha katika nafasi yako” Amesisitiza Waziri Ummy.

Aidha umemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani kumpeleka taarifa kuhusu utendaji kazi wa Mhandisi huyo ili aweze kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kuwa ndio mshauri Mkuu wa ujenzi huo.

Majaliwa aagiza kukamilika kwa mradi wa maji kifura
Hili ndo agizo la wakunga na wauguzi nchini