Mshambuliaji kutoka nchini Ureno, Ricardo Jorge Vaz Tê, ameonekana akifanya mazoezi na kikosi cha West Bromwich Albion, baada ya kumalizana na klabu ya Akhisar Belediyespor ya nchini Uturuki.

Uchunguzi uliofanywa na kituo cha televisheni cha Sky Sports, umebaini uongozi wa klabu ya West Brom upo katika mipango ya kutaka kumuongeza Vaz Te kwenye kikosi chao, kutokana na mazungumzo yayoendelea baina ya pande hizo mbili.

Vaz Te, mwenye umri wa miaka 28 ana fursa ya kipekee ya kusajiliwa na klabu yoyote kwa sasa nchini England, kutokana na kanuni za ligi kuu ya nchi hiyo kumruhusu kufanya hivyo kwa kutumia kigezo cha kuwa mchezaji huru.

Vaz Te, aliwahi kucheza soka nchini Engalnd akiwa na klabu ya Bolton Wanderers kati ya mwaka 2003–2010, na kisha alijiunga na West Ham Utd kabla ya kuruhusiwa kuondoka mwanzoni mwa mwaka huu na kutimikia nchini Uturuki.

Sababu kubwa iliyomuondoa Vaz Te, kwenye kikosi cha West Ham Utd ilikua ni majeraha ya mara kwa mara ambayo yalimnyima nafasi ya kucheza kama alivyokua anatarajiwa na wengi.

Akiwa na West Ham Utd alifanikiwa kucheza michezo 51 ya ligi kuu na kufunga mabao 15.

Ligi Daraja La Kwanza Bara Kuanza Sept 19
Yanga Yapewa Masharti Ya Kufanya Uchaguzi