Mtandao wa kijamii WhatsApp inayomilikiwa na kampuni ya Facebook, imekataa ombi la Serikali ya India kutaka kila ujumbe wa WhatsApp kuwekewa alama ya utambulisho, ili iwe rahisi nchini humo kufuatilia na kumfahamu mtumiaji wa kwanza lengo ikiwa ni kudhibiti uhalifu.

Serikali ya India inatafuta njia mbadala ya kufuatilia mawasiliano ya watumiaji wa mitandao ya kijamii hasa mtandao wa WhatsApp ambao una watumiaji wengi zaidi nchini humo.

Serikali ya India inasema ipo tayari kushirikiana na WhatsApp kutengeneza njia hiyo ambayo haitaingilia mawasiliano baina ya mtumiaji mmoja na mwingine, ili kudumisha Sera ya WhatsApp ya kutoingilia mawasiliano ya watumiaji wake.

WhatsApp inayomilikiwa na Kampuni ya Facebook ina watumiaji hai zaidi ya milioni 400 nchini India pekee.


Wezi ‘wampiga’ Beyonce, waondoka na Sh. 2 bilioni
Rais Samia afanya uteuzi