Msanii wa filamu Bongo na mwanamitindo, Jacqueline Wolper kupitia kurasa wake wa instagram ametoa shukrani zake kwa kumaliza mwaka kwa baraka tele zikiwemo kutarajia kufunga ndoa hivi karibuni na hivyo ameona ni vyema aweke wazi mipango hiyo.

Kupitia ujumbe huo mrefu aliouchora kwenye kurasa wake wa instagram Wolper hajaweka wazi kuhusu mume wake mtarajiwa na kuwaambia mashabiki wake wasihangaike kumjua ni  mwanaume gani kwani hatumii mtandao wa instagram.

” Sema sasa wambea msijichoshe huyu sasa hayupo insta wala hajui haya mambo”. amesema Wolper.

Licha ya kutomtaja mpenzi wake Wolper amechukua nafasi hiyo kumtolea povu mmakonde wake Harmonize kwa kumsaliti na kumdharau.

”Pamoja na kuwa alishatokea mmakonde na kunipeleka mpaka mtwara na matembele nikachuma na wanakijiji kunipokea na kupikia familia na kutambulishwa kwa wazazi lakini sikufanikiwa kufikia hatua hii ambayo wewe umefika” ameandika Wolper

Wolper ameendelea kwa kusema ”Wewe ni mwanaume ambae umejitoa ili tu niwe wako,umetaka tufike mbali kwanza kabla ya mambo mengine (uwende kwa wazazi, (NDOA) pamoja na kwamba mahusiano yangu ya nyuma yalikuwa yana misukosuko mingi ila umemthamini Jacq. Nilipotoka niliteswa sana na mapenzi yaani usaliti, dharau, kukosa na mapenz ya dhati”

Pia ameongeza kuwa katika mahusiano amejifunza kunyamaza bila kuyaweka hadharani na siku ya leo ndipo anatarajia kumtambulisha nyumbani kwao, Moshi na taratibu nyingine kama mahari kufuata.

Majaliwa awaweka kitimoto viongozi Tanesco
Polepole: Hakuna kiongozi anayetishiwa